TIBA YA BAWASIRI BILA UPASUAJI
Bawasiri ni ugonjwa gani? Bawasiri ni nini?
Bawasiri au Kikundu au Puru ni hali ya kuvimba kwa mishipa ya damu katika njia ya haja kubwa. Kwa Kiingereza hujulikana kama Hemorrhoid au Piles.
Katika hatua yake ya kuonekana wazi ugonjwa hujitokeza kama uvimbe au vivimbe kadhaa kwenye maeneo ya tundu la haja kubwa.
Karibu katika kila watu wanne watu watatu kati yao wanasumbuliwa na ugonjwa huu. Ni ugonjwa wa pili kati ya magonjwa yanayosumbuwa watu wengi zaidi duniani baada ya U.T.I
Kutokana na sehemu au mahali hasa ugonjwa wenyewe unapojitokeza umepelekea watu wengi kuwa na aibu kujisema kwamba wanaumwa ugonjwa huu.
Tatizo la bawasiri linaonekana kuwawapata kirahisi zaidi wanawake kuliko wanaume.
Bawasiri husababishwa na nini?
Watu wengi wamekuwa wakijiuliza ugonjwa wa bawasiri husababishwa na nini.
Bawasiri ni ishara inayokuambia kwenye mfumo wako wa mmeng’enyo wa chakula kuna kitu hakipo sawa.
Bawasiri ni tatizo linaloanzia kwenye mfumo wa mmeng'enyo wa chakula. Huu mfumo ukishakua mbovu unakupelekea kutokupata choo vizuri, unaanza kupata choo kigumu sana wakati mwingine unaweza kukaa siku kadhaa bila kupata choo kabisa.
Mfumo wako dhaifu wa mmeng'enyo wa chakula ndiyo sababu ya chakula kupita bila kumeng’enywa vizuri kwenye utumbo mdogo.
Hivyo chakula kinapitiliza kwenda moja kwa moja kama kilivyo kwenye utumbo mkubwa ambako maji maji ya kwenye chakula hufyonzwa na kuacha chakula kikiwa kikavu.
Utakapotaka kupata choo, choo hutokea kikiwa kikavu jambo linalokulazimu kutumia nguvu nyingi kukisukuma choo kitoke.
Nguvu hii unayoitumia wakati unapata choo ndiyo sababu ya kutanuka kwa misuli na kupelekea kukwanguliwa na choo kigumu na pole pole utaanza kuona kinyama kinajitengeneza, na kufuatiwa na maumivu na miwasho kwa ndani, na wakati mwingine unapata kilichoambatana na damu.
Unapoendelea kupata choo kigumu kwa kipindi kirefu misuli nayo huendelea kukwanguliwa na kinyama huongezeka mpaka kinatokea nje na kufanya bawasiri ya nje.
Ukiona unamaliza siku nzima hujapata choo au wakati mwingine inapita siku mbili au tatu au zaidi na hupati choo ni dalili mbaya sana kwa afya yako.
Vyovyote itakavyokuwa hakikisha kila siku unapata choo japo mara moja au mpaka mara tatu lakini isipite siku nzima hujapata choo.
Choo kiwe kilaini na usitumie nguvu nyingi ili kukipata na hata ikitokea choo kilaini sana tuseme unaharisha mara moja au mbili kwa wiki bado ni ishara una afya nzuri.
Choo unachopata kiwe ni kirefu ukubwa wa ndizi na kisiwe kinachokatikakatika kama kile cha mbuzi.
Vitu vifuatavyo vinatajwa kama sababu zinazoweza kukusababishia ugonjwa huu.
Visababishi vya bawasiri:
1. Kufunga choo au kupata choo kigumu kwa muda mrefu
2. Ujauzito – wakati wa ujauzito watu wengine wanaweza kupatwa na bawasiri sababu ya msukumo wa mtoto karibu na sehemu ya kutolea haja kubwa
3. Kushiriki mapenzi kinyume na maumbile
4. Uzee – kadri miaka inavyosogea ndivyo inavyokuwa rahisi kwako kupatwa na ugonjwa huu kwa baadhi ya watu
5. Sababu za kurithi – baadhi ya watu wanaweza kurithi udhaifu wa ukuta huo wa njia haja kubwa ingawa ni asilimia ndogo sana.
6. Kuharisha sana kwa muda mrefu
7. Kutumia vyoo vya kukaa
8. Kunyanyua vyuma vizito
9. Mfadhaiko unaodumu muda mrefu (stress)
10. Uzito na unene kupita kiasi nk
11. Kutokula matunda kila siku
12. Kutokula mboga nyingi za majani kila siku
13. Kutokunywa maji mengi kila siku
14. Kukaa muda mrefu kwenye kiti
15. Kula ugali wa sembe
16. Kula wali kila siku
17. Kutokula chakula cha kutosha chenye nyuzinyuzi (faiba)
Dalili za bawasiri
Bawasiri dalili zake zinaweza kufanana kidogo na dalili za mtu anayeanza kuumwa vidonda vya tumbo. Nazo ni pamoja na zifuatazo :
1. Maumivu wakati wa kujisaidia haja kubwa
2. Kinyesi kunuka damu wakati wa kujisaidia
3. Muwasho sehemu ya tundu la haja kubwa
4. Uvimbe au kinyama kujitokeza sehemu ya tundu la haja kubwa
5. Haja kubwa yaweza kujitokea tu muda wowote
6. Kupungukiwa damu
7. Baada ya kupata haja kubwa unaweza usiishi tumbo kupungua
8. Maambukizi
Unapoona kuna damu inavuja mahala pa haja kubwa ama unapotoa haja, basi nashauri nenda haraka hospital kuonana na Daktari na kufanya vipimo, hasa kama tatizo ni limekutokea kwa mara ya kwanza.
Hata hivyo siyo kila kuvuja kwa damu kwenye sehemu ya haja kubwa inaweza kuwa ni bawasiri, wakati mwingine yaweza kuwa ni dalili za Saratani ya utumbo mpana.
AINA ZA BAWASIRI
Bawasiri imegawanyika mara 2. Kuna bawasiri ya ndani na bawasiri ya nje
1. Bawasiri ya ndani – Hii ni bawasiri ambayo inajitokeza ndani ya mfereji wa haja kubwa na kwa kawaida mgonjwa anaweza asihisi maumivu yoyote hivyo huwafanya watu wengi kutotambua kuwa wana ugonjwa huu.
Bawasiri ya ndani nayo imegawanyika katika hatua nne tofauti ambazo ni:
(a) Bawasiri ambayo haitoki mahali pake (bawasiri iliyosimama).
(b) Bawasiri ambayo wakati wa haja kubwa inatoka lakini baada ya kumaliza haja kubwa inarudi yenyewe ndani.
(c) Bawasiri ambayo wakati wa haja kubwa inatoka na hairudi tena ndani yenyewe bila kurudishwa na mgonjwa.
(d) Bawasiri inayotoka wakati wa haja kubwa na kubaki nje hata kama mgonjwa atairudisha bado itaendelea kubaki tu nje.
2. Bawasiri ya nje – Hii ni aina ya bawasiri ambayo hutokea eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa. Huwa na kiuvimbe au viuvimbe kadhaa na mara nyingi huambatana na maumivu na muwasho katika sehemu hiyo.
Kwa kawaida mishipa hiyo ya damu (vena) karibu na nje ya tundu la haja kubwa hupasuka na damu huganda.
MADHARA YA BAWASIRI
Zifuatazo ni athari za bawasiri kwa watu wa jinsia zote mbili:
• Upungufu wa damu mwilini
• Maumivu makali wakati wa kujisaidia haja kubwa
• Kuna uwezekano mkubwa wa kupata saratani ya utumbo (Cancer) sababu kile kinyama kinakaa kama kidonda na bila kutibika kwa muda mrefu
• Kuishiwa hamu ya tendo la ndoa
• Kupunguwa kwa nguvu za kiume
• Kushuka kwa ubora wa mbegu za mwanaume
• Kuvurugika kisaikolojia
• Kutokwa na kinyesi bila kujitambua
• Kushuka kwa uwezo wako wa kujiamini
• Kupungukiwa na uwezo wa kufanya kazi kutokana na maumivu
DAWA ya bawasiri bila upasuaji > Muanzima Asili
Matibabu ya bawasiri hutegemea na aina ya bawasiri.
Mara nyingi wagonjwa wa bawasiri hupatiwa tiba ya kukatwa kinyama (upasuaji) na kushauriwa kuendelea na tiba ya vyakula hata hivyo tiba huwa haina matokeo mazuri kwani baada ya muda tatizo hurudi tena kutokana na ukweli kuwa wanakuwa hawajatibu chanzo cha tatizo.
Hivyo tiba nzuri ya bawasiri ni kutumia dawa itakayotibu chanzo cha tatizo ndani ya mfumo wa mmeng’enyo wa chakula huku ukiendelea na tiba ya chakula.
Jambo la kwanza kabla ya tiba mgonjwa anapaswa kutibiwa tatizo la kutopata choo vizuri ikiwa analo kwa sababu hali hii huzidisha ugonjwa wa bawasiri.
Mgonjwa wa bawasiri pia aepuke kula nyama hasa ya ngombe, pilipili, maziwa na vitu vikali.
Muanzima Asili ni Tiba ya bawasiri bila upasuaji ya asili ya mitishamba ambayo:
*Inarekebisha matatizo yoyote kwenye mfumo wa mmeng’enyo wa chakula
*Inauongezea kasi mfumo wa mmeng’enyo wa chakula
*Ina nyuzinyuzi (faiba) nyingi ambayo ni mhimu kwa mtu yeyote anayesumbuliwa na bawasiri
*Inatibu aina zote za bawasiri
*Inaondoa tatizo la kufunga choo na kupata choo kigumu
*Pole pole kadri unavyoendelea kuitumia inaondoa kinyama kinachojitokeza sehemu ya haja kubwa kama matokeo ya bawasiri
*Ni dawa nzuri dhidi ya bakteria, virusi na vijidudu nyemelezi sifa ambazo zinayafanya kuwa bora kwa kutibu bawasiri.
0 Comments