Wakati mwingine wanandoa wanaweza wakawa wanatafuta mtoto, lakini wakawa wanakosea padogo sana ili kupata mtoto. Mazingira hayo yamekuwa na athari hizi na zile katika ndoa na wakati mwingine ndoa zimevunjika kutokana na tatizo ambalo kumbe kama wanandoa wangekuwa na elimu nalo lisingetokea.
Daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake kutoka H ospitali ya Mwananyamala jijini Dar es S alaam, Phabian Tumai, katika mazungumzo maalumu na gazeti hili anasema wanawake wengi hawajui kuhesabu mzunguko wao wa hedhi na namna unavyoweza kutumika katika kuleta au kutoleta ujauzito. H ata hivyo, daktari anaweka angalizo kwamba ili mfumo wa hedhi uwe na maana mintarafu suala zima la mimba kuna uhusiano na hali ya mfumo wa maisha ya mhusika, vyakula anavyokula na shughuli zingine za kawaida.
Mizunguko mitatu ya hedhi
Dk Tuimai anasema hedhi unaweza kuigawa katika mafungu matatu ambayo ni mzunguko mfupi (siku 21), mzunguko wa kati au kawaida (siku 28) na mzunguko mrefu wenye siku 35.
Kwa hapa mzunguko huanzia pale mwanamke anapoanza kupata damu za hedhi. Mbali na mizunguko hiyo ambayo haibadiliki badiliki, Dk Tumai anasema wapo wanawake wanaopata mizunguko ambayo haipo katika kundi hilo kwa maana ya kuanzia siku 22, 23, 24, 25, 26, 27, 29, 30, 31, 32, 33 na 34. Daktari anasema mwanamke anayepata mzunguko chini ya siku 21 na zaidi ya siku 35 anachukuliwa kwamba ana tatizo la hedhi. Kutokana na utofauti wa mizunguko kwa kila mwanamke, Dk Tumai anasema uanguliwaji wa yai ambao ndio kitu muhimu sana cha kuangalia mintarafu suala zima la mimba, pia hutofautiana.
“ Ili mwanamke aweze kujua siku zake sahihi za hatari ni lazima ajue anaangua yai siku gani au siku ya ngapi kutokana na urefu wa mzunguko wake,” anasema. Anasema mzunguko rahisi kufuatilia ni ule usiobadilika badilika. “ Wapo wanawake ambao wao tangu wanaanza kupata damu ya hedhi basi siku zake hazibadiliki badiliki na wapo wale ambao wao kila mwezi tarehe hubadilika badilika,” anafafanua.
Daktari anasema wimbi kubwa la wanawake wamejikita kwenye chati inayozunguka mitandaoni inayoonesha jinsi ya kuhesabu siku za hatari na kujua mzunguko wao lakini anasema chati hiyo haimfai kila mwanamke. “ Chati hizo nyingi ni zile za mzunguko wa siku 28 ambao wengi wapo kwenye mzunguko huo, lakini hata hivyo haimaanishi kila mwanamke atumie chati hiyo kwa kuwa suala hili ni sawa na msemo wa kila mbuzi hula kulingana na urefu wa kamba yake,” anasema.
Kupevuka kwa yai ni nini? Dk Tumai anasema kupevuka kwa yai (ovulation) ni pale yai moja au zaidi yanapoachiwa kutoka kwenye moja ya mfuko wa mayai (ovary) na hii hutokea mwishoni mwa muda ambao mwanamke ana uwezo wa kupata mimba katikati ya mzunguko wake wa hedhi. Kila mwezi, kati ya mayai 15 hadi 20 huzalishwa ndani ya mfuko wa mayai ya mwanamke. Y ai lililopevuka hutolewa na kusukumwa kwenye mirija ya uzazi ( fallopian tubes) inayounganisha ‘ ovari’ na tumbo la uzazi.
Mifuko ya uzazi sio kwamba inapokezana kutoa yai kila mwezi. H ili hutokea bila mpangilio maalumu.
Lini utapata mimba?
Ili kupata ujauzito kwa njia ya kawaida, yai na mbegu kutoka kwa mwanamume lazima vikutane kwenye mirija ya uzazi. Y ai la mwanamke haliwezi kuwa hai kwa zaidi ya saa 24 baada ya kuwa kwenye upevushaji, kwa hiyo kukutana kwa yai na mbegu lazima kutokee ndani ya muda huo.
Kwa upande mwingine, mbegu za mwanamume huweza kuwa hai hadi kufikia siku saba. Mbegu zitaishi kwa raha tu kwenye uke, mfuko wa mimba, au kwenye mirija ya uzazi kwa muda wote huo. H ii inamaanisha, sio lazima mwanamke ahesabu muda sahihi kabisa ikiwa yai limepevushwa kupata ujauzito. Kiuhalisia kila mwanamke ana jumla ya siku sita kwenye mzunguko wake wa hedhi ambazo anaweza akashika mimba.
Kwa hiyo kama akifanya tendo la ndoa katika kipindi hiki, yai lake lililopevuka tayari linaweza likakutana na mbegu yenye afya ya mwanamume na kupevushwa.
Ni wakati gani upevushaji hutokea?
Dk Tumai anasema upevushaji mara nyingi hutokea kati ya siku ya 12 hadi 14 kabla ya hedhi nyingine kuanza. H ii ni wastani tu wa makadirio, hivyo inaweza ikawa ni siku chache kabla au baada. Kwa mfano, tuseme mwanamke ana mzunguko wa kawaida wa hedhi wa siku 28.
Anatakiwa kuhesabu siku ya kwanza ya kuona hedhi yake kama siku ya kwanza na kwamba siku hiyo hadi ya tisa si hatari kwake isipokuwa kuanzia siku ya 10 hadi ya 15 ndio hatari kwake kuweza kupata mimba. H ata hivyo, wanawake wengi wana mizunguko inayotofautiana. Y ai linaweza kupevuka wiki moja kabla au baada kutoka mwezi mmoja hadi mwingine.
Dalili za kupevuka yai ni zipi?
Kuhusu dalili, Dk Tumai anasema mwanamke anaweza kuona dalili za yai kupevuka kwa karibu siku tano kabla. Anasema dalili kuu na viashiria vya yai kupevuka ni pamoja na mabadiliko ya ute kwenye mlango wa uzazi na kuongezeka joto la mwili.
Dalili zingine ni maumivu ya tumbo, kujaa maziwa na kupata maumivu kwenye maziwa. Mwanamke pia anaweza kuwa na dalili ya kuumwa kiuno, mgongo na baadhi hutokwa chunusi usoni au uso kutakata isivyo kawaida. H alikadhalika kuna wanaoumwa tumbo na hata kuharisha na kuwa na hamu ya kushiriki tendo la ndoa kuliko kawaida.
Mabadiliko ya ute
Akifafanua zaidi, Dk Tumai anasema ute wa mlango wa uzazi ni uteute anaouona mwanamke kwenye nguo ya ndani au kwenye karatasi laini (tissue) anapokwenda kujisaidia haja ndogo.
Anasema mabadiliko ya ute wa mlango wa uzazi ni alama ya kuwa mwanamke yupo kwenye dirisha la kuweza kupata mimba. B aada ya hedhi kuisha ute wa mlango wa kizazi huongezeka kwa ujazo na hubadilika pia hali yake. Mabadiliko haya yanaendana na kuongezeka kwa kiwango cha homoni ya oestrogen mwilini.
Mwanamke atakuwa zaidi kwenye uwezo wa kupata mimba kama uteute unakuwa hauna rangi, unateleza sana na unavutika. Ute huo hufanana na sehemu nyeupe ya yai ukilivunja. Kazi ya uteute huu ni kusaidia mbegu kuwa na spidi zaidi wakati zinaogelea kuelekea kwenye mfuko wa kizazi. H alikadhlika huilisha na kuilinda mbegu inapokuwa inasafiri kuelekea kwenye mirija ya uzazi kukutana na yai.
Maumivu ya tumbo
Kwa mujibu wa Dk Tumai, mwanamke mmoja kati ya watano huwa anasikia kitu kinaendelea kwenye mifuko yao ya mayai ( ovaries) wakati wa kipindi cha upevushaji.
H aya ni pamoja na maumivu madogo madogo au yanayovuta na kuachia. Mwanamke akizihisi dalili hizi katika kipindi kilekile kila mwezi, aangalie uteute wa mlango wake wa kizazi.
Hisia za tendo la ndoa
H isia hizi ni dalili nyingine na mwanamke wakati mwingine huwa muongeaji zaidi au kutamani kuongea na wanaume. Mwanamke pia akijiona ngozi inakuwa laini kuliko kawaida na kujihisi kuwa na mvuto zaidi kimwonekano ni dalili pia. S ambamba na hilo, hata harufu ya mwili ya mwanamke huwa nzuri pia inayovutia wanamume katika kipindi hiki.
Kuongeza uwezo wa kupata mimba
Kama unatafuta mtoto, jaribu kukutana na mumeo kila baada ya siku mbili au tatu. Mbegu zenye uogeleaji mzuri zitakuwa sehemu husika siku yoyote ukiwa kwenye upevushaji. Tendo la ndoa la mara kwa mara kwenye mzunguko wako wote ni hatua inayokupa uwezo mkubwa wa kushika ujauzito. Kufanya tendo la ndoa wakati mlango wa kizazi chako una uteute ni wakati unaoongeza uwezo wako wa kupata ujauzito. L a kuzingatia ni kwamba, utumiaji wa mzunguko wa hedhi ni njia moja wapo ya asili ya kujikinga na mimba zisizotarajiwa au njia ya kupanga kuzaa
Jinsi ya kupata mapacha
👇👇👇👇👇👇👇
Jinsi ya kupata watoto wa like tu ingia hapa link 1
0 Comments