Header Ads Widget

DALILI ZA VIDONDA VYA TUMBO ZINAZOCHANGIA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

Baadhi ya dalili za vidonda vya tumbo zinazopelekea pia upungufu wa nguvu za kiume ni pamoja na zifuatazo:
1. Kuchoka choka sana bila sababu maalum
2. Kuumwa mgongo au kiuno
3. Kizunguzungu
4. Kukosa usingizi
5. Kiungulia
6. Tumbo kujaa gesi
7. Tumbo kuwaka moto
8. Maumivu makali sehemu kilipo kidonda
9. Kukosa choo au kupata choo kwa shida tena kikiwa kigumu na chenye kukatika kama cha mbuzi
10. Kusahahu sahau na
11. Hasira bila sababu.
Dalili au matatizo yote hayo hapo juu yanayompata mgonjwa wa vidonda vya tumbo ndizo ambazo kwa namna nyingine kama matokeo yake zinapelekea tatizo la Upungufu wa nguvu za kiume kwa wanaume wengi.
Mwanaume anayesumbuliwa na vidonda vya tumbo pia anaweza kupatwa na kupungukiwa nguvu za kiume kama matokeo hasi ya baadhi ya dawa za kemikali zinazotumika kutibu vidonda vya tumbo, ingawa madaktari huangalia zaidi matokeo chanya ya dawa kuliko matokeo hasi hasa inapobidi upone ugonjwa mwingine hatari zaidi hata kama moja ya matokeo yake hasi yaweza kuwa ni kupatwa na ugonjwa mwingine.
Kuna uhusiano mkubwa kati ya vidonda vya tumbo na msongo wa mawazo au huzuni. Na msongo wa mawazo au stress moja kwa moja husababisha kushuka kwa nguvu za kiume!
Kwa kifupi Mwanaume fanya kila uwezalo usiuguwe vidonda vya tumbo au fanya kila njia kuhakikisha unajitibia vidonda vya tumbo hadi unapona ikiwa unataka kuendelea kulinda heshima yako nyumbani.

Post a Comment

0 Comments